Morris Kimuli ameapishwa rasmi kuwa mwakilishi wa chama cha mawakili nchini LSK kwenye jopo la kuwatafuta makamishna wapya wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC.
Haya yanajiri siku moja baada ya rais Uhuru Kenyatta kubatilisha uteuzi wa Dorothy Jemator kufuatia mgogoro kwenye chama hicho.
Kimuli ameapishwa kwenye shughuli iliyoongozwa na jaji mkuu Martha Koome katika mahakama ya upeo.
Jaji Mkuu Martha Koome amelitaka jopo hilo linaloongozwa na Dr. Elizabeth Muli kuhakikisha kuwa zoezi la kujaza nafasi hizo nne za makamishna wa IEBC linaendeshwa kwa njia huru na wazi.
Watu 669 wametuma maombi kujaza nafasi hizo akiwemo meneja wa mawasiliano katika tume hiyo ya IEBC Tabitha Mutemi, aliyekuwa naibu mwenyekiti wa tume ya ardhi nchini NLC Abigael Mbagaya na mawakili Alice Yano, Harriette Chiggai na Norman Magaya.