Afisa yeyote wa Polisi anayekabiliwa na hali ya msongo wa mawazo anashauriwa kutafuta usaidizi katika idara ya Polisi wakati wowote.
Wito huu unatolewa na Inspekta wa Polisi Hillary Mutyambai ambaye anasisitiza kwamba idara hiyo iko radhi kushughulikia matatizo yote ya kiakili kwa maafisa wake.
Mutyambai amesema haya akijibu maswali kutoka kwa Wakenya waliotaka kujua iwapo kuna lolote linalofanywa na idara ya Polisi kushughulikia matatizo ya msongo wa mawazo kufuatia kuongezeka kwa visa vya mauji miongoni mwa Polisi.
Tukio la hivi pundeni ambapo afisa wa GSU Hudson Wakise alimuua kwa kumpiga risasi mkewe Pauline Wakasa ambaye pia alikuwa afisa wa trafiki na kisha kujiua kufuatia mzozo wa kinyumbani.