Muwaniaji wa urais Dr. Mukhisa Kitui amejipata mashakani kufuatia madai kwamba alimpiga mwanamke mmoja mjini Mombasa.
Malalamishi yaliyowasilishwa kwa Polisi na mwanamke anayetambulika kama Diana Opemi Lutta yanadai kuwa aliumizwa na Dr. Mukhisa Kituyi Mei 22 katika hoteli moja mjini Mombasa.
Kufuatia madai hayo, Inspekta wa Polisi Hillary Mutyambai amemuagiza kamanda wa Polisi katika eneo la Pwani kuanzisha uchunguzi na kuwasilisha faili kwa mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.
Mwanamke huyo alipiga ripoti katika kituo cha Polisi cha Nyali ambapo alipewa fomu ya P3 kutafuta matibabu kutokana na majeraha anayodai kupata wakati wa vurugu na mwanasiasa huyo.
Diana amedai kuwa Dr. Mukhisa Kituyi ni mchumba wake.