Mochari za kaunti ya Kisumu zimepewa muda wa saa 48 kuondoa au kuzika miili yote waliyohifadhi la sivyo wanyanganywe leseni zao.
Waziri wa Afya katika kaunti hiyo Boaz Otieno anasema hatua ya miili kuendelea kukaa katika hifadhi hizo inachangia watu kukiuka masharti ya kuzuia msambao wa virusi wa corona.
Familia zinazopoteza wapendwa wao zimetakiwa kuzika wapendwa wao kwa muda wa saa 48 ilivyoagiza serikali.
Kaunti hiyo imekuwa ikirekodi idadi kubwa ya visa vya corona katika siku za hivi karibuni, wananchi wakilaumiwa kwa kukosa kuzingatia masharti yaliyowekwa.
Kaunti hiyo inapambana na aina mpya ya virusi vya corona kutoka India vilivyoletwa nchini na wasafiri wanane.