Mfanyibiashara Bashir Mohamed aliyepotea takribani siku kumi zilizopita alinyongwa kwa kutumia mikono hadi kufa umebaini upasuaji.
Uchunguzi wa maiti yake umedhibitisha kuwepo kwa ushahidi unaonesha kuwa marehemu aliteswa kabla ya kukata roho.
Maiti yake ilikuwa na dalili za kuchomwa huku kichwa chake kikiwa na majeraha ya kugongwa kwa kutumia kifaa butu.
Vile vile, makucha ya vidole vyake yalionekana kuondolewa kwa mujibu wa upasuaji huo uliofanywa na mpasuaji mkuu wa serikali Johansen Oduor.
Mwili huo ulipatikana Jumamosi iliyopita katika mto Nyamindi kaunti ya Kirinyaga na watu waliokuwa wameenda kuoga.









