Mchezaji wa zamani wa raga Alex Olaba amekamatwa kwa madai ya kujaribu kumuua shahidi kwenye kesi ya ubakaji inayomkabili.
Olaba na mshtakiwa mwenza Frank Wanyama wanakabiliwa na mashtaka ya kumbaka kwa zamu msichana mmoja na waliachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000.
Polisi walimshika Olaba huko Nairobi West alipokuwa anakutana na afisa wa upelelezi kupanga njama ya kumuangamiza shahidi kwenye kesi hiyo.
Mchezaji huyo wa zamani alikuwa ametafuta usaidizi kuhusu atakavyomuua shahidi huyo ambapo Polisi waliambiwa na kumuwekea mtego ambao hatimaye umemnasa.
Polisi walipoambiwa walimtuma mpelelezi wa siri aliyejifanya kuwa angemsaidia kumuua shahidi huyo na hivyo wakamtia mbaroni wakati wa mkutano huo.
Pindi aliposhikwa, Olaba aliwaambia Polisi kwamba alikuwa ameshambuliwa na mapepo ya kishetani.