Mary Juma Deya mjane wa mhubiri aliyekumbwa na utata wa ‘miracle babies’ Gilbert Deya ameripotiwa kufariki dunia baada ya mwili wake kupatikana nyumbani kwake eneo la bondo kaunti ya Siaya.
Kifo chake kilidhibitishwa na taarifa ya polisi huku kiini chake kikichunguzwa.
Kwa mujibu wa mkuu wa kituo cha polisi cha Bondo Robert Aboki kisa hicho kiliripotiwa Jumapili tarehe 16 Machi 2026 jioni mwanafamilia alipoenda kumwangalia baada ya kutoonekana kwa muda.
‘‘Jana mwendo wa saa 4:45 jioni, Erick Orido alienda kumjulia hali Mary Deya. Mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani na alipobisha hakukuwa na jibu,’’ Aboki alisema.
Mwili wa mwendazake ulipatikana ndani ya nyumba yake baada ya wanafamilia na majirani kuvunja na kuingia alipokosa kujibu bisho mlangoni.
Kifo chake kinajiri miezi tisa baada ya kifo cha mumewe aliyeaga kupitia ajali ya barabarani.
Mhubiri Deya aligonga vichwa vya habari vya kimataifa kufuatia kashfa ya kuwawezesha wanandoa wasiokuwa na uwezo kupata watoto kwa njia tatanishi iliyopelekea uchunguzi wa kitaifa na kimataifa kuhusu chanzo cha watoto hao na hata kushtakiwa kwa ulanguzi wa binadamu.









