Baada ya kupata kibali cha tume ya huduma za mahakama (JSC) sawa na bunge, Martha Koome anatarajiwa kuapishwa rasmi kuwa mwanamke wa kwanza Jaji Mkuu Ijumaa.
Hafla ya kumuapisha Koome kwa wadhifa huo itaandaliwa katika Ikulu ya rais Nairobi kabla yake kufululiza moja kwa moja hadi katika afisi zake zilizoko katika mahakama ya upeo.
Watakaompokea Koome katika mahakama ya upeo ni kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji wa mahakama ya upeo pamoja na msajili wa mahakama Anne Amadi.
Mwilu ambaye amekuwa kaimu Jaji Mkuu tangu kustaafu kwa David Maraga Januari 12, 2021 atamkabithi rasmi mikoba Koome Jumatatu ijayo.