Aliyekuwa mbunge wa Gem Jakoyo Midiwo atazikwa nyumbani kwake Akala, kaunti ya Siaya Jumamosi hii, Juni 26.
Haya yamesemwa na nduguye Dr. George Midiwo ambaye ametaja kwamba kamati za mazishi zinakutana Nairobi na Kisumu kupanga mipangilio ya kumpumzisha marehemu.
Nduguye mwanasiasa huyo ameongeza kwamba wanashauriana na serikali kuhusu namna mazishi hayo yataendeshwa kuambatana na masharti ya usalama kuzuia msambao wa ugonjwa wa corona.
Jakoyo Midiwo alivuta pumzi ya mwisho Juni 14 akiwa Nairobi Hospital alipokimbizwa kwa matibabu ya dharura.
Dadake mkubwa Julia Apiyo aliyefariki Juni 3 alipewa buriani Jumamosi iliyopita nyumbani kwake Nyadhi, Alego Usonga









