Mashirika mbalimbali ya kijamii yamewakashifu viongozi wakuu serikalini kwa madai ya kuishambulia idara ya mahakama baada ya majaji watano kuharamisha mchakato wa BBI.
Mashirika hayo ikiwemo tume ya kutetea haki za kibinadamu KHRC chini ya afisa mkuu mtendaji Davis Malombe na MUHURI wanatoa witoa wito kwa viongozi kuheshimu uamuzi huo wa mahakama na kukata rufaa iwapo hawaridhiki nao.
Viongozi wa mashirika hayo akiwemo Khelef Khalifa wa MUHURI wanasema idara ya mahakama ndiyo inayomwokoa mwananchi wa chini wakati anakandamizwa na inafaa kuheshimiwa sawia na idara zingine huru.









