Mahakama na EACC kushirikiana kupambana na ufisadi

0

Mahakama zitapatia kipau mbele kushughulikia na kumalizia zaidi ya kesi 400 za ufisadi ili kurejesha mali iliyoibwa inayogharimu Sh11b.

Hakikisho hili limetolewa na Jaji Mkuu Martha Koome baada ya kukutana na afisa mkuu mtendaji wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC Twalib Mbarak.

Koome ametoa changamoto kwa majaji kubeba mzigo binafsi wa kuwa na mbinu zitakazohakikisha kwamba kesi hizo za ufisadi zimeharakishwa.

Mkutano huo umelenga kuangazia namna idara ya mahakama na EACC watashirikiana kuhakikisha kwamba vita dhidi ya ufisadi vimefaulu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here