Kenya yapewa mkopo mwingine na Benki ya Dunia

0

Kenya itapewa mkopo mwingine wa Sh14b kutoka kwa Benki ya Dunia kusaidia katika kununua chanjo ya corona.

Katika taarifa, Benki ya Dunia imesema chanjo hiyo inatazamiwa kununuliwa kupitia mpango unaojumuisha mataifa mbalimbali ya Afrika wa COVAX.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba ufadhili huo utasaidia Kenya kuchukua hatua makhususi kufanikisha vita dhidi ya janga hilo la corona.

Haya yanajiri chini ya majuma mawili baada ya Kenya kupewa mkopo mwingine wa Sh80b kutoka kwa Benki ya Dunia kutumika katika kukomboa uchumi uliotatizika kutokana na janga la corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here