JSC yaanza kumtafuta mrithi wa Maraga

0

Kibarua cha kumtafuta mrithi wa David Maraga kwa wadhifa wa jaji mkuu kimeanza rasmi Jumatatu huku jaji Said Juma Chitembwe akiwa wa kwanza kuhojiwa na tume ya huduma za mahakama (JSC).

Jaji Chitembwe,54, aliyechaguliwa jaji wa mahakama kuu miaka kumi na miwili iliyopita amesema yuko katika nafasi nzuri ya kuwarithi watungulizi wake Dkt. Willy Mutunga na David Maraga kwa sababu ya uzoefu wake katika idara ya mahakama.

Amesema alichangia pakubwa katika kupunguza mrundiko wa kesi mahakamani alipohudumu katika mahakama za Kakamega, Malindi, Marsabit na Migori.

Jaji Chitembwe kuhakikisha kuwa kesi za ufisadi zinasikilizwa kwa haraka kinyume na ilivyo kwa sasa ambapo zinachukua muda mrefu.

Watu 10 wameorodheshwa kuhojiwa kwa wadhifa huo akiwemo majaji; Nduma Nderi, William Ouko, Martha Koome, Marete Njagi na mawakili Philip Murgor, Fredrick Ngatia, Patricia Mbote, Moni Wekesa na Alice Yano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here