Jaji ajitoa kwenye kesi ya mwanajeshi aliyeua familia yake Laikipia

0

Jaji Florence Muchemi amejiondoa kwenye kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa mwanajeshi Peter Mugure kwa misingi kwamba amewahi shughulikia kesi nyingine inayomhusu mshukiwa.

Mwanajeshi huyo anatuhumiwa kumuua mkewe Joyce Syombua na watoto wao wawili Prince Michael na Shanice Maua katika kambi ya jeshi ya Laikipia.

Jaji Muchemi amesema alishughulikia kesi inayomhusu mshukiwa mwenza wa Mugure Collins Pamba ambaye sasa ni shahidi wa serikali.

Pamba ambaye wakati huo alikuwa mfanyikazi katika kambi hiyo ya jeshi alikubali kumsaidia Mugure kubeba na kusafirisha miili hiyo mitatu na kuizika.

Na sasa Jaji huyo ameelekeza kesi hiyo kusikilizwa na mwenzake Abigail Mshilla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here