Mahakama itaendelea kutoa hukumu ya kifo kwa watakaopatikana na hatia kufanya makosa yanayoambatana na kifungo cha kifo.
Mahakama ya upeo chini ya rais wake Jaji Mkuu Martha Koome imetoa mwelekeo huo kufuata uamuzi wa mahakama kuu ulioharamisha hukumu ya kifo kwenye kesi maarufu ya Francis Muruatetu.
Jaji Koome hata hivyo ameelekeza kuwa kesi ya Muruatetu inahusishwa na kesi za mauaji pekee.
Mahakama hiyo ya upeo vile vile imezielekeza asasi husika za kisheria ikiwemo bunge pamoja na mwanasheria mkuu kutathmini uamuzi huo kwa makusudi ya kubaini hatima ya hukumu ya kifo na hukumu ya maisha.
Kwenye kesi hiyo ya mwaka 2017, Francis Muruatetu pamoja na mshtakiwa mwenza Wilson Mwangi walikataka rufaa dhidi ya hukumu ya kifo dhidi yao baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mfanyibiashara mmoja uamuzi ambao ulibatilishwa na mahakama kuu na kuwa hukumu ya maisha.