Mahakama Alhamisi alasiri itatoa uamuzi kuhusu kesi inayopinga marekebisho ya katiba kupitia BBI.
Uamuzi huo wa saa nane na nusu utatolewa na jopo la majaji watano Joel Ngugi, George Odunga, Jarius Ngaah, Janet Mulwa na Chacha Mwita
Majaji hao walitoa agizo linalozuia tume ya uchaguzi IEBC kuendelea mbele na mipango ya kuandaa kura ya maamuzi mpaka kesi hiyo isikilizwe na kuamuliwa.
Kamati inayoongoza mchakato huo wa BBI imeelezea matumaini yake kwamba mahakama itawapa Wakenya fursa ya kuelekea katika kura ya maamuzi itakapotoa maamuzi yake.
Wenyekiti wenza wa kamati hiyo Dennis Waweru na Junet Mohamed wamesema mahakama pekee ndio imesalia kizingiti kwa Wakenya kushiriki kwa kura ya maamuzi baada ya mabunge kupitisha mswada huo