Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA limeondoa marufuku iliyowekwa dhidi ya taifa la Kenya mwezi wa Februri mwaka huu.
FIFA Kupitia barua kwa katibu mkuu wa shirikisho la Soka humu nchini FKF Barry Otieno limesema litatuma ujumbe humu nchini kujadili hatua za kurejesha Kenya katika soka ya kimataifa..
Ktaibu mkuu wa Shirikisho hilo Fatma Samoura aidha amesema wataandaa mkutano na waziri wa Spoti Ababu Namwamba kuhusu maswala ya usimamizi wa soka humu nchini.
Kenya ilipigwa marufuku baada ya vuta nkuvute kati ya FKF ikiongozwa na Nick Mwendwa na waziri wa Michezo wa zamani Amina Mohammed.