EPRA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta

0
Meneja Mkurugenzi wa EPRA Daniel Bargoria

Imeandikwa na Faith Kendi

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) imetangaza kuwa bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa hazitabadilika kwa kipindi Cha mwezi wa Machi na Aprili.

“Katika kipindi Cha Mwezi wa Machi na Aprili bei ya mafuta haitabadilika. Jijini Nairobi, Super Petrol, Dizeli na Mafuta ya Taa sasa zitauzwa kwa shilingi 178.28, shilingi 166.54 na shilingi 152.78 kwa siku 30 zijazo,” EPRA imetangaza.

Tangazo hili linajiri huku kukiwa na wasiwasi kuhusu Bei ya bidhaa za petroli kutokana na vita vinavyoendelea kwenye eneo la Mashariki ya kati.

Kulingana na taarifa iliyotolewa tarehe 14 Machi 2026, Bei ya super Petrol itaendelea kuuzwa kwa shilingi 178.28 kwa lita, Dizeli kwa Ksh166.54, na Mafuta ya Taa kwa shilingi 152.78 jijini Nairobi.

Jijini Mombasa, Bei ya Super Petrol itaendelea kuuzwa kwa shilingi 175.00 kwa lita, Dizeli kwa shilingi 163.26, na Mafuta ya Taa kwa shilingi 149.49.

Jijini Kisumu bei ya Super Petrol, Dizeli, na Mafuta ya Taa yatauzwa kwa shilingi 178.16, shilingi 166.76, na shilingi 153.03 kwa lita na kule Jijini Eldoret bei ya Super Petrol, Dizeli, na Mafuta ya Taa yatauzwa kwa shilingi 178.16, shilingi 166.77, na shilingi 153.03 kwa lita moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here