COTU yapinga mipango ya Safaricom kuwafuta kazi wafanyikazi

0

Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU umepinga vikali mipango ya kampuni ya mawasiliano nchini Safaricom kuwafuta kazi baadhi ya wafanyikazi wake.

Katika taarifa, katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli amesema mipango hiyo imezua sintofahamu na wasiwasi miongoni mwa wafanyikazi takribani elfu sita wa kampuni hiyo.

Atwoli anasema mipango hiyo inayoongozwa na afisa mkuu mtendaji Peter Ndegwa inakiuka haki za wafanyikazi hao ambao anasema bidii yao kazini imechangia ufanisi wa kampuni hiyo kubwa ya mawasiliano nchini.

COTU sasa inataka bodi ya usimamizi wa Safaricom kumfuta kazi Ndegwa iwapo hatalinda haki za wafanyikazi.

Inadaiwa kuwa wengi wa wafanyikazi wa Safaricom wametakiwa kutuma maombi yao upya ya kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here