Caroline Kangogo, polisi mwanamke anayedaiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi wanaume wawili akiwemo afisa mwenzake John Ogweno chini ya saa Ishirini na nne anatafutwa.
Kangogo anadaiwa kumpiga risasi Ogweno akiwa kwenye gari lake katika kituo cha Polisi cha Nakuru Jumatatu na kisha kutoroka na bastola yale aina ya Ceska.
Sku moja baadaye anaarifiwa kumuua kwa kumpiga risasi mwanamme mwingine huko Juja baada ya kukukomboa naye hoteli.
Taarifa ya idara ya upelelezi DCI inaonesha kwamba Kangogo aliondoka kwenye chumba alimokuwa na marehemu usiku wa manane na kuacha mwili wake kwenye damu.
Wafanyikazi wa hoteli hiyo wanasema hawakusikia mvurugano wa aina yoyote kwenye chumba waliomokuwa wawili hao.