Aliyekuwa waziri wa fedha Henry Rotich ameshtakiwa upya kuhusiana na sakata ya mabilion ya pesa katika ujenzi wa mabwawa ya Arror na Kimwarer.
Rotich amefikishwa mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya kupambana na ufisadi ya Milimani Douglas Ogoti ambapo amesomewa upya mashtaka ya wizi wa mali ya umma, utumizi mbaya wa afisi na kukosa kuwajibika.
Hata hivyo waliokuwa washukiwa wenza Kamau Thugge na Susana Koech ambao ni makatibu wa zamani katika wizara hiyo wameondolewa mashtaka.
Badala yake upande wa mashtaka umeimabia mahakama kuwa inalenga kuwatumia wawili hao kuwa mashaidi dhidi ya Rotich ambaye ni mkubwa wao wa zamani.
Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma pia imeondoa majina ya watu 20, raia wa Italia ambao hawajahi kufika mahakamani kufunguliwa mashtaka.









