Afisa mkuu wa Afya kaunti ya Nakuru afariki kutokana na makali ya corona

0

Afisa Mkuu wa huduma za afya ya umma katika kaunti ya Nakuru amefariki kutokana na makali ya virusi vya Corona.

Akidhibitisha taarifa hizo, Gavana Lee Kinyanjui amesema kuwa Samwel Kingori amefariki akipokea matibabu hospitalini baada ya kuonyesha dalili za Corona.

Katika rambirambi zake kwa familia, Gavana Kinyanjui amemtaja mwendazake kama afisa aliyejitolea katika kazi yake ili kuendeleza sekta ya afya katika kaunti hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here