NAIBU GAVANA WA KISII ROBERT MONDA ATIMULIWA

0

Naibu Gavana wa Kaunti ya Kisii Robert Monda amebanduliwa afisini kufuatia madai ya kuhusika katika ufisadi.

Monda ametimuliwa na wawakilishi wadi wa Kaunti hio jioni ya leo baada ya wawakilishi wadi 53 kupiga kura kuunga mkono hoja iliyowasilishwa na mwakilishi wadi wa Ichuni Wycliffe Siocha.

Naibu huyo wa Gavana Simba arati alikabiliwa na madai ya matumizi mabaya ya afisi na kupokea hongo ili kumpa ajira jamaa aliyetambuliwa kama Denis Misati madai aliyoyakana akihoji kuwa alipokea fedha kutoka jamaa huyo kama malipo ya mkopo aliyokuwa amempa hapo awali.

‘Baba ya Misati ni rafiki familia yangu. Nilimkopesha fedha na aliponitembelea yeye na familia yake nilimuomba kulipa mkopo huo. Aliagiza wanawe pamoja na mkewe kumsaidia kulipa mkopo huo ndiposa nikapokea fedha kutoka kwa mwanawe Denis Misati’’ Alijitetea Naibu Gavana.

Fedha hizo zinadaiwa kutumiwa kushawishi kuajiriwa kwa Misati kwa kampuni ya usambazaji maji ya Kisii GWASCO.

Haya yalizuka baada ya sehemu ya pesa hizo kutumwa kwa Bi Lucy Muthoni, mkurugenzi mkuu wa Gwasco.

Niabu Gavana huyo sasa anatarajiwa kufika mbele ya bunge la Sneti kujitetea dhidi ya madai hayo.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Naibu Gavana kujipata mbele ya Seneti wa hivi majuzi kuponea mikononi mwa maseneta akiwa ni Naibu Gavana wa Siaya William Oduol

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here