MSHUKIWA WA MAUAJI JOHN MATARA AFUNGULIWA MASHTAKA MAPYA

0

Mshukiwa mkuu kwenye mauaji ya mwanasosholisti Starlet Wahu, John Matara amewasilishwa katika mahakama ya Ruiru hii leo kwa madai ya ubakaji na wizi wa kimabavu.

Akifikishwa mbele ya hakimu Charles Mwaniki, Matara amedaiwa kutekeleza kosa hilo mnamo mwezi Mei mwaka jana.

Matara anadaiwa kumuibia Nekesa Wangila shilingi 88,300, kuchukua kitambulisho cahke cha kitaifa na paspoti katika eneo la Kahawa Wendani akiwa amejihami na kisu.

Hata hivyo, Matara amekanusha mashtaka yote dhidi yake na kupitia wakili wake Samuel Ayora kutaka kuwachiliwa kwa dhamana akidai kuhangaishwa na makachero wa DCI na hivyo kuhitaji kupata huduma za kimatibabu.

Hakimu Mwaniki ameagiza aandikishe taarifa katika kituo cha polisi cha Ruiru kuhusu madai hayo pamoja na kupelekwa hospitalini huku kesi hiyo ikiratibiwa kutajwa tena siku ya Ijumaa atakapo baini iwapo atawachiliwa kwa dhamana au la.

Hii ni mwezi moja tu baada ya Matara kukana mashtaka ya kumuua Wahu alipofikishwa mbele ya jaji Kanyi Kimondo wa mahakama kuu ya Nairobi na kuzuiliwa katika gereza la Industrial Area.

Kushtakiwa kwa Matara hii leo kunatokana na uchunguzi wa polisi kufuatia madai ya ubakaji na wizi kutoka kwa wanawake kadhaa dhidi yake kutoka eneo la Kasarani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here