Wakili Fred Ngatia ahojiwa kwa nafasi ya jaji mkuu

0

Hii leo ni zamu ya wakili Fred Ngatia kuhojiwa na tume ya huduma za mahakama JSC kwa nafasi ya jaji mkuu.

Ngatia ambaye anapigiwa upatu kumrithi David Maraga anatazamiwa kuelezea makamishna wa JSC mbona ni yeye anafaa zaid na wala si wenzake tisa.

Wakili huyo mtajika anatazamiwa kukabiliwa na wakati mgumu kujibu maswali mbalimbali kuhusu utendakazi wake.

Mahojiano hayo yanayofanyika katika mahakama ya upeo yanaendelea kwa sasa .

Ngatia ameahidi kuhakikisha kuwa kesi zinasikilizwa na kuamuliwa kwa wakati iwapo atateuliwa kuwa jaji mkuu ili kuharakisha zoezi la upatikanaji wa haki.

Hapo jana, Jaji wa Mahakama ya Leba Nduma Nderi alihojiwa na tume hiyo ambapo aliahidi, miongoni mwa masuala mnegine kupambana na ufisadi katika idara ya mahakama iwapo atateuliwa kumrithi Maraga aliyestaafu mapema mwaka huu.

Wengine ambao watahojiwa wiki hii ni jaji William Ouko, Profesa Moni Wekesa na Alice Yano.

Wiki iliyopita, watu watano walihojiwa akiwemo wakili Philip Murgor, Jaji David Marete, jaji Martha Koome, msomi Profesa Kameri Mbote na jaji Juma Chitembwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here