POLISI WAMSAKA MWANAUME ALIYETEKELEZA MAUAJI HOMA BAY.

0

Maafisa wa polisi kaunti ya Homa Bay wanamsaka mwanaume mmoja anayedaiwa kumuua mpenziwe mwenye umri wa miaka 28 kufuatia mzozo wa kimapenzi.

Marehemu Mary Kwamboka alipatikana ameuawa  nyumbani kwake eneo la Rodi Kopan’y siku ya jumapili .

Uchunguzi wa polisi umeonyesha kuwa marehehemu alikuwa nyumbani pamoja na mwanaume anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa zamani siku ya jumamosi kabla ya mzozo huo.

Kulingana na majirani hakuna anayejua kilichotokea baada ya hapo mpaka siku ya jumapili walipopatwa na wasiwasi na kwenda kumwangalia.

“Kama majirani tulipatwa na wasiwasi manake haikuwa tabia ya Kwamboka kunyamaza hivo. Tulipofungua mlango wake ,tulimpata akiwa amezingirwa na damu na amefariki,” mmoja wa majirani amesema.

Kamanda wa DCI kaunti hiyo Abed Kavoo amesema kuwa wawili hao walikuwa wameachana ila mwanaume  huyo alitembelea marehemu siku ya jumamosi kabla yake kupatikana akiwa amekufa.

Kisu anachodaiwa kutumia mwanaume huyo kilipatika katika eneo la mauaji hayo na kiko mikononi mwa polisi.

“Tunaendelea kumtafuta mshukiwa huyo aliyetoroka baada ya mauaji hayo,” Kavoo amesema.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika mochwari ya hospitali ya rufaa ya Homa bay.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here