Mwanaume wa miaka 46 amefariki baada ya kukatwa na panga na mpenziwe wa siri katika kijiji cha Mukimwani lokesheni ya Kalimoni kaunti ya Makueni.
Justus Manthi Kyengo alikumbana na mauti yake hapo jana, Jumapili, nyumbani kwa mpenziwe Christine Wanza Mutie mwenye umri wa miaka 46,
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, wawili hao walitofautiana kabla ya mshukiwa kuchukua panga na kumkata mpenziwe, akisaidiwa na mwanawe wa miaka Nicholas Mutinda Mutie mwenye umri wa miaka 20.
Kamanda wa polisi Makueni Joseph Ole Napeiyana anasema mwili wa mwendazake ulikuwa na mjeraha ya panga kwa shingo, kichwa na mkono wa kulia.
Wanakijiji wanasema mumewe mshukiwa anafanya kazi katika kaunti ya Nairobi sawia na mkewe marehemu.