Mahojiano ya kumtafuta jaji wa mahakama ya upeo yaanza rasmi

0

Mahojiano ya kumtafuta jaji wa mahakama ya upeo kujaza nafasi yake Jackton Ojwang aliyestaafu yanaanza asubuhi hii.

Tume ya huduma za mahakama JSC chini ya uenyekiti wa Olive Mugenda inaendesha mahojiano hayo ya siku tatu ambapo watu saba watahojiwa.

Hii leo ni zamu ya majaji Said Juma Chitembwe na D.K Njagi Marete kuhojiwa. Hapo kesho, itakuwa zamu yao jaji Nduma Nderi wa mahakama ya leba na msomi Dr Patrick Nyaberi Lumumba.

Wengine ambao watahojiwa ni majaji William Ouko, Joseph Sergon na wakili Alice Yano.

Mahojiano haya yanafanyika baada ya kutamatika kwa yale ya kumtafuta jaji mkuu na tayari Martha Koome amependekezwa kuteuliwa kumrithi David Maraga na anasubiri kupigwa msasa na bunge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here