Kikosi Cha Tatu Cha Wanajeshi Wa Kenya Chatumwa DRC.

0

Taifa la Kenya limetuma kikosi cha tatu cha wanajeshi wa kudumisha amani katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC)

Kikosi hicho kinajiunga na wenzao walioondoka humu nchini wiki mbili zilizopita chini ya mwavuli wa Jeshi la Kikanda la  Afrika Mashariki (EACRF) lililojukumiwa kukabiliana na makundi ya waasi nchini DRC.

Akizungumza alipoaga wanajeshi hao Naibu Kamanda wa Jeshi La Nchi Kavu Meja Jenerali Peter Muteti amesifia kikosi cha kwanza akisema wamepiga hatua kubwa katika kurejesha  amani D.R.C.

Meja Jenarali aidha amesihi wanajeshi hao kua kielelezo na mabalozi bora wa Jeshi la    Kenya (KDF) .

KDF ni Kikosi cha kitaaluma, cha kuaminika, chenye uwezo wa misheni na tunajivunia uwezo wetu. Tunaposema wewe ni mshale, tunamaanisha kwa vile tunakuamini.  Twataka mdumishe kauli mbiu yetu ya Utayari kwa huduma ,” alisema Naibu Kamanda.

Meja Jenerali huyo aidha alirai majeshi ya Kenya kuzingatia sheria na kulinda haki za msingi za kibinadamu wanapoendesha shughuli zao DRC.

Kenya iliahidi kutuma zaidi ya wanajeshi mia tisa kujiunga na EACRF watakaosaidia wanajeshi wa DRC kupambana na makundi ya waasi ikiwemo M23.

Jeshi la Kikanda linatarajiwa kuziba muanya uliowachwa baada ya kuondoka kwa  kikosi cha UN Cha Kulinda Amani DRC (MONUSCO ).

MONUSCO hivi majuzi imekashifiwa na wenyeji wa Mashariki Mwa DRC kwa kula njama na waasi, kutesa vijana na kukiuka haki za wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here