Mahakama kuu ya Nyeri imeahirisha vikao vya kuskilizwa kwa kesi ya aliyekuwa afisa wa jeshi Peter Mugure anayedaiwa kuua mpenziwe na watoto wake wawili.
Akitoa mwelekeo kwenye kesi hiyo, Hakimu Florence Muchemi ameagiza mshukiwa kufikishwa mahakamani tarehe 11 Aprili mwaka huu wakati kesi hiyo itaanza kuskilizwa.
Mshukiwa amewasilisha ombi la kutaka kujiwasilisha kwenye kesi hiyo badala ya kuwakilishwa na mawakili.
Mugure anatuhumiwa kumuua mkewe Joyce Syombua na wanawe wawili mwaka wa 2019 katika kambi ya jeshi Nyanyuki.