Nancy Kabui aidhinishwa kuwa mkaguzi mkuu wa hesabu za umma

0

Nancy Kabui Gathungu ameidhinishwa kumrithi Edward Ouko kama mkaguzi mkuu wa hesabu za umma baada ya uteuzi wake kuidhinishwa na bunge.

 Wabunge akiwemo Aden Duale na Junet Muhamed walisifia utendakazi wa Edward Ouko huku wakielezea matumaini yao kwamba Kabui ataendelea na alipoachia mtangulizi wake.

Spika wa bunge hilo Justine Muturi atarejesha jina lake kwa rais Uhuru Kenyatta kwa uteuzi rasmi ambapo atahudumu kwa muda wa miaka minane pasipo muhula huo kuongezwa.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here