Visa vipya 461 vya corona vyaripotiwa Kenya

0

Idadi ya visa vya corona hapa nchini imefikia 11,252 baada ya watu 461 kupatikana na ugonjwa huo katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

 Katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman anasema idadi hiyo imeongezeka baada ya kupima sampuli 4,261.

Wagonjwa wengine 51 wamepona na kufikisha idadi hiyo kuwa 3,068 huku watu wengine saba wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo na kufikisha 209 idadi ya waliofariki kufikia sasa.

Msambao wa visa hivyo kote nchini, Nairobi 248, Machakos 97, Kiambu 20, Kajiado 15, Migori 14, Busia 12, Nakuru 11, Laikipia 7, Nyeri 7, Kilifi 6, Lamu 4, Uasin Gishu 4, Kakamega 3, Kisii 3, Kisumu 2, Makueni 2, Mombasa 1, Taita Taveta 1 na Bomet 1.

 Wahudumu wanne wa afya wamepoteza maisha baada ya kuambukizwa virusi vya corona.

Katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman anasema wahudumu wengine wapatao 450 wameambukizwa ugonjwa huo wakiwa kazini.

Amesema serikali inafanya kila iwezalo kuwalinda wahudumu wa afya ikiwemo kuwapa vifaa vinavyohitajika ikiwemo magwanda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here