Magoha awasomea wazazi kuhusu ulezi wa watoto

0

Waziri wa elimu Profesa George Magoha amewalaumu wazazi kufuatia kuongezeka kwa visa vya unywaji pombe na utumizi wa mihadarati miongoni mwa wanafunzi.

Profesa Magoha amesema licha ya serikali kuweka mikakati inayolenga kukomesha utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi, jukumu kuu linasalia kwa wazazi kuwajibikia vilivyo ulezi bora.

Waziri Magoha amesema haya wakati wa uzinduzi mwongozo wa kitaifa utakaotumika kukomesha matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here