Kamati ya Leba kwenye bunge la seneti imewaagiza Waziri wa fedha John Mbadi, Waziri wa vyama vya ushirika Wycliffe Oparanya na Meneja Mkurugenzi wa shirika la reli (KRC) Phillip Mainga kufika mbele yake kueleza sababu ya kucheleweshwa kwa malpo ya wafanyikazi waliostaafu wa shirika la reli la Kenya
Kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Pokot Magharibi Julius Murgor imemwonya watatu hao kuwa iwapo hawatafika kwenye kikao hicho watatozwa faini ya shilingi elfu 500
Mbadi anatarajiwa kutoa maelezo kuhusu malipo ya shilingi bilioni 2.6 kwa madiwani wa zamani na pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu elfu 11,900 wakiwemo waliokuwa wafanyikazi wa shirika la reli
Ikumbukwe awali Waziri Mbadi amekosa kuhudhuria vikao viwili mfululizo kikiwemo kile cha Julai 31 na Agosti 4 2025.









