Uhuru akiuka itifaki, amkaribisha Odinga kuongea

0

Rais Uhuru Kenyatta amevunja itifaki na kumkaribisha kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuhutubu kwenye sherehe za Madaraka Dei.

Kinyume na desturi za maadhimisho ya kitaifa, rais Kenyatta alimkaribisha Odinga kuhutubu baada ya naibu wake William Ruto ambapo alitumia fursa hiyo kuwarai Wakenya kukumbatia umoja huku akipigia debe BBI.

Wakati uo huo

Rais Uhuru Kenyatta alilazimika kukatiza hotuba yake ya Madaraka Dei kwa muda baada ya jamaa mmoja kujaribu kumkaribia.

Iliwalazimu maafisa wa usalama wa rais kumzuilia jamaa huyo ambaye alikuwa miguu mitupu na kumbeba hobela hobela na rais kuendelea na hotuba yake.

Hii ni mara ya tatu chini ya mwezi mmoja kwa mtu kujaribu kumfikia rais ikiwemo hivi maajuzi huko Lucky Summer, Nairobi ambapo msafara wa rais ulilazimika kusimama kumuondoa barabarani jamaa aliyetaka kumuona rais Kenyatta.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here