RAIA WATANO WA SUDAN WAKAMATWA KWA KIFO CHA KUTATANISHA CHA ‘MAMA FUA’ HUKO KILIMANI

0

 

Watu watano wenye asili ya taifa la Sudan wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilimani hapa jijini Nairobi baada ya kukamatwa kufuatia kifo cha mwanamke mmoja aliyeenda kuwafanyia usafi nyumbani kwao

Mwanamke huyo ametambuliwa kuwa Zaituni Kavaya mwenye umri wa miaka 54 mkazi wa mtaa wa Kibra

Kulingana na mwanawe, Faith Kavaya, alielezwa kwamba mamake alikuwa ameanguka kutoka kweny ghorofa ya tano ya jumba alikokuwa ameenda kufanya usafi

Hata hivyo inaarifiwa kuwa mwanamke huyo alitofautiana na Raia hao wa Sudan kuhusu kupotea kwa shilingi elfu tano zilizokuwa kwenye mojawapo ya nguo alizokuwa akiosha

Katika harakati hizo mwanamke huyo alijaribu kutoroka ambapo alianguka kutoka ghorofa ya tano na kufariki dunia

Ripoti ya upasuaji imebainisha kuwa alifariki kutokana na majeraha kadhaa aliyopata kutokana na kugongwa na kifaa butu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here