Mkuu wa idhaa ya Biblia Husema Broadcasting Douglas Omariba amefunga ndoa katika hafla ya kufana iliyoandaliwa Ijumaa tarehe 19 Disemba 2025.
Katika hafla iliyohudhuriwa na mamia ya jamaa na marafiki, Omariba anayefahamika zaidi kama Omari amerasmisha mahusiano yake na mpenziwe wa muda mrefu Christine Mangi.
Wawili hao walianza kuchumbiana wakiwa wafanyikazi wa kituo cha Biblia Husema Broadcasting.
“Mbele ya umati huu na mbele ya mwenyezi Mungu naapa kukupenda, kukuenzi ” alisema Omariba.
Hafla hio aidha ilijawa ucheshi Christine akimtania mchumba wake.
“Nitakupa bega la kulilia na kuvuta machozi yako kila wakati na hasa wakati ambapo timu unayoienzi ya Manchester United itakapopigwa.” Alisema Christine semi iliyoangua kicheko miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo.
Harusi hiyo imehudhuriwa na wafanyikazi wa BHB wakiongozwa na Meneja Msimamizi Victor Mandala.
Mashabiki wa Kituo cha Truth FM chini ya Muungano wao wa Victory Family na wale wa Biblia Husema chini ya muungano wao wa BHB Blessed Family.









