TSC kuajiri walimu elfu tano Julai mwaka huu

0

Tume ya huduma za walimu imetangaza kuwa itaajiri walimu zaidi ya elfu tano kuanzia mwezi wa saba mwaka huu.

Katika taarifa, afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia amesema hatua hiyo inalenga kusaidia kupunguza uhaba wa walimu katika shule za umma nchini.

Tume hiyo pia inapanga kuajiri walimu wanafunzi elfu sita baada ya hazina ya kitaifa kuwatengea billion 2.5 kuajiri walimu, mwaka ujao wa kifedha.

Hatua hiyo pia inalenga kusaidia serikali katika kufanikisha mafunzo ya mtaala mpya wa elimu, CBC.

Macharia anasema hadi kufikia sasa, wametoa mafunzo kwa walimu zaidi ya elfu mia moja kuhusiana na mtaala huo mpya, hazina ya kitaifa pia ikitenga shilingi billion moja kwa ajili ya shughuli hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here