Kamati ya bunge la seneti kuhusu kawi imepewa muda wa majuma mawili kufanya uchunguzi kuhusiana na bei za mafuta na kuwasilisha ripoti yake bungeni.
Maseneta wakiongozwa na George Khaniri wa Vihiga wamelalamikia hatua ya tume ya kudhibiti kawi nchini EPRA kuendelea kuongeza bei ya mafuta hali ambayo wanasema imechangia kuongezeka kwa gharama ya maisha.
Hata hivyo wameitaka serikali kuangazia maisha ya mwananchi wa kawaida kwa sababu wengi wanateseka kutokana na bei ghali ya nauli na bidha ambayo imeadhiri uchumi .
Katika bei za mafuta ambazo zilitangazwa Ijumaa wiki iliyopita, EPRA iliongeza bei ya mafutu ya petrol kwa shilingi Sh3.56 na sasa itauzwa kwa shilingi 126.37, diseli inauzwa shilingi 107.66 na mafuta taa shilingi 97.85.









