Rais Ruto asifia mpango wa Uhuru wa Linda Mama

0

Rais William Ruto ameutetea mpango wa afya wa Linda Mama chini ya uongozi wa mtangulizi wake rais mstaafu Uhuru Kenyatta kama ulioweka msingi wa mipango ya afya iliyoboreshwa.

 Akizungumza siku ya Juma nne katika chuo kikuu cha Umma kaunti ya Kajiado rais Ruto alisisitiza kuwa ufanisi wa mpango huo wa awali ulichochea kuanzishwa kwa mpango wa sasa wa Linda Jamii ambao alisema umezidisha utoaji huduma hadi kwa familia nzima kinyume na mama pekee ilivyokuwa awali.

“Tulijifunza mengi kutoka kwa mpango wa Linda Mama na kutokana na tajriba hiyo tukaunda mpango wa Linda Jamii ambao ulikuwa uboreshaji wa mpango wa Linda Mama. Linda Mama ilikuwa nzuri, Linda Jamii ni bora zaidi,” Rais alieleza.

‘’Tunafaa kuwa wakarimu kwake, mpango wa Linda Mama ulikuwa mpango mzuri.’’

Mpango wa Linda Mama ulianzishwa na utawala wa rais Kenyatta ukitoa huduma ya bure kwa akina mama waja wazito kwa madhumuni ya kuwahakikishia upatikanaji wa huduma muhimu za afya pamoja na watoto wanaojifungua.

Kwa mujibu wa amiri jeshi mkuu mpango huo mpya unaendana sambamba na ajenda ya serikali ya Huduma ya Afya kwa wote (UHC) ambayo inalenga kuhakikisha kuwa kila mkenya anaweza kupata matibabu pasi na kukabiliwa na changamoto za kifedha.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here