Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini kiko katika asilimia 8.4% baada ya maambukizi mapya 488 kudhibitishwa kati ya sampuli 5,831 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita .
Wizara ya afya inasema hii inafikisha 174,773 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini wakati ambapo Busia imejiunga na Kisumu na Nairobi kwa kuwa miongoni mwa kaunti zinazoandikisha maambukizi mapya kupindukia.
Idadi ya waliopona imefikia 119,589 baada ya kupona kwa watu 343 huku waliofariki wakifikia 3,378 kufuatia maafa ya wagonjwa wengine 16.
Jumla ya watu 1,095,122 wamepata chanjo ya corona huku waliopata dozi ya pili wakiwa 110,052 wakiwemo wahudumu wa afya 33,425.









