John Cox Lorionokou ameapishwa rasmi Jumatatu tarehe 13 Oktoba 2025 kuwa msajili mpya wa vyama vya kisiasa.
Cox aliyeteuliwa na rais William Ruto mapema mwezi Oktoba 2025 amejaza rasmi pengo la ofisi hiyo lililoachwa wazi na mtangulizi wake Ann Nderitu baada ya kupata fursa ya kuwa kamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC).
Lorionokou atakayehudumu kwa muda wa miaka sita katika wadhifa huo ameahidi kuboresha demokrasia ndani ya vyama vya kisiasa.
Akiongoza hafla hiyo katika mahakama ya upeo, jaji mkuu Martha Koome amemtaka Lorionokou kuangazia zaidi mkondo bora wa vyama vya kisiasa alivyovitaja kuwa vyombo vinavyochangia kufaulu kwa demokrasia ya taifa.
Sawia katika hafla hiyo aliapishwa pia Agatha Wahome kuwa naibu msajili wa vyama vya kisiasa ili kufanya kazi pamoja na Lorionokou.