Mahakama yatia breki usajili wa polisi

0

Mahakama ya Uajiri na Leba imesitisha zoezi la usajili wa makurutu kujiunga na vikosi vya polisi kutokana na kesi iliyowasilsihwa dhidi yake.

Katika kesi hiyo mlalamishi John Harun Mwau alitaka kutatuliwa kwa mzozo wa majukumu baina ya Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi (NPSC) na Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS).

Hakimu Hellen Wasilwa Alhamisi tarehe 2 Septemba 2025 alitoa agizo la muda la kuzuia shughuli hiyo kufuatia kesi iliyowasilishwa tarehe 30 Septemba 2025.

Agizo hilo lilitolewa siku moja kabla ya kuanza kwa usajili, jaji Wasilwa akielekeza pande husika katika kesi hiyo iliyoratibiwa kutajwa tarehe 21 Octoba 2025 kuwasilisha majibu ndani ya siku saba.

Zoezi hilo la siku tano lilikuwa limetangazwa na Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) kufanyika katika vituo 416 vya usajili kote nchini makurutu 10, 000 wapya wakilengwa kusajiliwa.

Agizo hilo la mahakama lilijiri kufuatia majuma kadhaa ya vuta ni kuvute baina ya NPSC na NPS kuhusu mchakato wa usajili wa makurutu.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here