Mahakama Kutoa Uamuzi Kuhusu Shughuli ya Usajili wa Makurutu

0

Mahakama Jumanne tarehe 21 Oktoba, 2025 inatarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu shughuli ya usajili wa makurutu elfu 10 kote nchini uliokuwa uanze Oktoba tarehe 3,2025.

Mahakama ya Leba ilisitisha usajili wa makurutu wa polisi kufuatia mvutano kuhusu nani kati ya Inspekta Jenerali wa polisi na tume ya huduma za polisi NPSC ana mamlaka ya kuendesha shughuli hiyo.

Hii ni baada ya mwanasiasa John Harun Mwau kuwasilisha kesi akidai kwamba Katiba ya Kenya inatambua huduma ya polisi NPS kuwa chini ya uongozi huru wa Inspekta Jenirali wa polisi na kwamba hakuna mtu au chombo chochote chenye mamlaka ya kumwagiza kuhusu maswala ya ajira, uhamisho, upandishwaji vyeo au kusimamishwa kazi kwa maafisa wa polisi.

Jaji Hellen Wasilwa wa mahakama ya uhusiano wa ajira na kazi alitoa amri ya kusitisha usajili huo kwa muda hadi pale kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa kikamilifu.

Pia hatua ya NPSC kuanzisha mchakato wa uajiri ni kinyume na katiba kwani ni Inspekta Jenerali pekee aliye na mamlaka ya kuongoza maswala ya ndani ya huduma ya polisi

Mahakama iliagiza mawakili wa Mwau kuwakabidhi stakabdhi ya kesi washtakiwa wote kufikia leo ikiwemo Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja, huduma ya polisi NPS, tume ya kitaifa ya polisi NPSC na mwanasheria mkuu Dorcas Oduor.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here