Maafisa wa idara ya upelelezi nchini wanaendesha uchunguzi wa kuwanasa wezi ambao waliiba tingatinga kutoka kaunti ya Kitui na kuificha katika eneo la Ruiru, kaunti ya Kiambu.
Afisa mkuu wa uchunguzi katika kaunti hiyo Singi Nzioka anasema wanafanya kila wawezalo kuwanasa wezi hao ambao waliegesha tingatinga hiyo ndani ya boma la mtu katika eneo la Matinyani baada ya kuishiwa na mafuta.
Mmoja wa washukiwa anayewasaidia wachunguzi kuwanasa washukiwa anasema tingatinga hiyo ilisafirishwa na watu asiowajua ambao walidai kuwa walikuwa wanaipeleka kurekebishwa.