Polisi wametibua kampeini za muwaniaji huru Feisal Bader kujipigia debe kuwania kiti cha ubunge cha Msambweni kwenye uchaguzi mdogo utakaoandaliwa Disemba 15.
Muwaniaji huyo alikuwa ameandamana na wendani wa naibu rais William Ruto akiwemo Johnstone Muthama, Hassan Omar, Boni Khalwale na mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa ambapo walikuwa wananuia kuandaa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Ukunda.
Haijabainika mara moja kuhusu ni kwa nini Polisi wamezuia kuendelea kwa kampeini hizi ila inaarifiwa kuwa ni kutekelezwa kwa masharti yaliyowekwa na kamati ya usalama na kuidhinishwa na baraza la mawaziri ili kutuliza joto la kisiasa nchini.