Wendani wa Ruto wakutana Jubilee

0

Wabunge wapatao 38 wendani wa naibu rais William Ruto wamefanya mkutano wa faragha katika makao makuu ya chama tawala cha Jubilee jijini Nairobi.

Wakiongozwa na mbunge wa Kandara Alice Wahome, wanasiasa hao wamekana taarifa za hapo awali kwamba wanapanga kufanya mapinduzi katika chama hicho na badala yake kusema kuwa walikutana kujadili maswala yenye umuhimu kwa taifa hili.

Kuu kwenye ajenda ya mkutano huo uliongozwa na naibu rais William Ruto ilikuwa ni ushauri wa jaji mkuu David Maraga kwa rais Uhuru Kenyatta kwamba alivunje bunge sawa na chaguzi za mashinani za chama hicho.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here