Wauguzi waapa kuendelea mbele na mgomo wao

0

Wauguzi wanaogoma wameapa kuendelea na mgomo wao hata kama utadumu kwa mwaka mmoja iwapo masharti yao hayatatekelezwa.

Wahudumu hao wa afya wakiongozwa na naibu katibu mkuu wa chama cha Wauguzi nchini (KNUN) Maurice Opetu wamesema kitakachowafanya kurejea kazini ni iwapo serikali za kaunti zitatii masharti yao ya kutia saini makubaliano ya kurejea kazini.

Wauguzi hao aidha wamemtaka rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kutanzua mgomo huo ambao umesababisha wagonjwa kuendelea kutaabika kwa majuma kadhaa sasa.

Nao wauguzi katika kaunti ya Mombasa wakiongozwa na katibu wao Peter Maroko wameisuta serikali ya gavana Hassan Joho kwa kukosa kutilia maanani kilio chao.

Katika kaunti ya Taita Taveta,

Serikali ya Gavana Granton Samboja imewafuta kazi wauguzi na maafisa wa kliniki takribani mia tano walio mgomoni.

Katika notisi, serikali hiyo imewataka wahudumu hao wa afya kurejesha mali ya serikali wanayomilki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here