Wageni waalikwa pekee ndio wataruhusiwa kuingia katika uwanja wa Gusii Stadium wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Mashujaa Jumanne wiki ijayo.
Haya yamesema na kamati ya maanalizi ya sherehe za kitaifa chini ya uongozi wake katibu mkuu katika wizara ya usalama wa ndani Dkt. Karanja Kibicho ambaye amewaongoza wenzake kukagua uwanja huo hii leo.
Kibicho amesema sherehe za mwaka huu zitakuwa tofauti na zile zilizopita huku shamra shamra za kila siku zikipunguzwa kwa sababu ya corona.
Tayari rais Uhuru Kenyatta amekutana na viongozi wa kutoka eneo la Nyanza akiwemo gavana Ongwae na mwenzake wa Nyamira John Nyagarama katika Ikulu ya rais, Nairobi kabla ya maadhimisho hayo ya Octoba 20.
Taarifa kutoka Ikulu iliarifu kuwa mkutano huo ulijadili namna eneo la Gusii litafaidika pakubwa na maendeleo kutoka kwa serikali kuu.