Watu sita zaidi wafariki kutokana na Corona

0

Watu sita zaidi wamefariki baada ya kukutwa na virusi vya corona kwa muda wa saa ishirini na nne zilizopita.

Hii ina maana kuwa idadi ya maafa yaliyotokana na virusi hivyo yamepanda na kufikia 548.

Habari njema ni kuwa watu 217 wamepona virusi hivyo hatari na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 18, 670.

Taarifa kutoka wizara ya afya inaonyesha kuwa watu wengine 246 wamekutwa na virusi hivyo vya corona baada ya sampuli 4, 179 kuchunguzwa, na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 32, 364.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here